BAGHDAD: Maandamano kupinga kukaliwa kwa Iraq
10 Aprili 2005Matangazo
Wairaqi kwa maelfu wameandamana katika mji mkuu wa Iraq,Baghdad na miji mingi mingine,kupinga kuwepo kwa vikosi vya washirika,chini ya uongozi wa Marekani nchini Iraq.Maandamano hayo yameitishwa na mkuu wa kidini wa Kishia Moqtada al-Sadr na yamefanywa siku ya kuadhimishwa mwaka wa pili tangu kuangushwa kwa serikali ya Saddam Hussein.