Baghdad. Maafisa wanane wa polisi wauwawa katika shambulio dhidi ya kituo cha Polisi nchini Iraq.
25 Juni 2005Nchini Iraq wanamgambo wamewauwa maafisa wanane wa polisi katika shambulio dhidi ya kituo cha polisi karibu na mji wa R amadi, magharibi ya mji mkuu Baghdad.
Karibu na Kirkuk upande wa magharibi , mtu mmoja Mkurdi ambaye anafanyakazi katika kampuni la saruji la Marekani amepigwa risasi na kufa. Hii inafuatia shambulio la bomu la kujitoa muhanga siku ya Alhamis karibu na mji wa Fallujah dhidi ya magari ya kijeshi ya jeshi la Marekani ikiwa ni pamoja na wanajeshi wanawake.
Jeshi la Marekani limesema maiti mbili zimepatikana , nne nyingine hazijatambuliwa lakini wanafikiriwa kuwa wameuwawa. Miongoni mwa majeruhi 13, ni pamoja na wanajeshi wanawake 11.
Rais George Bush amesisitiza jana kuwa atapambana na wapiganaji wa chini kwa chini na kuwashinda nchini Iraq. Kura ya maoni inaonesha kuwa Wamarekani wanataka kufahamu muda maalum kwa ajili ya majeshi ya nchi hiyo kuondoka Iraq.
Akiwa ziarani nchini Marekani, waziri mkuu Ibrahim Jaafari amesema kuwa muungano wa vyama vinavyounda serikali unapata mafanikio hatua kwa hatua.