BAGHDAD : Kikao cha bunge la Iraq kufanyika Machi 16
6 Machi 2005Kikao cha kwanza cha bunge jipya la Iraq kufanyika tarehe 16 mwezi huu wa Machi.
Tarehe hiyo ni kumbukumbu ya miaka 17 ya kupigwa kwa mabomu ya kemikali kwa mji wa Wakurdi wa Halabja kaskazini mwa Iraq kulikofanywa na wanajeshi wa dikteta aliyeangushwa madarakani Saddam Hussein.
Kwa mujibu wa Naibu waziri mkuu na afisa mwandamizi wa Kikurdi Barham Saleh kikao hicho kitafanyika aidha serikali mpya iwe imeundwa au la.Saleh ameelezea matumaini yake kwamba wanasiasa watamaliza mzozano wao wa kuwania nyadhifa za juu kabla ya kuanza kwa kikao hicho cha bunge.
Kikao hicho kipya cha bunge kitamchaguwa spika mpya na baadae kulichaguwa baraza la rais ambalo ndilo litakalomchaguwa Waziri Mkuu.
Maafisa wa Iraq wanataraji kikao hicho kitaweza kurudisha utulivu kutokana na machafuko ya uwamgaji damu yanayoendelea.