BAGHDAD: Jalal Talaban achaguliwa rais wa Iraq
6 Aprili 2005Matangazo
Bunge la Iraq limemchagua rais mpya katika kikao chake cha nne hii leo tangu kufanyika uchaguzi wa Januari 30.
Rais Ghazi Al Yawar anayeondoka madarakani ambaye ni msunni ameteuliwa kuwa makamu wa rais.
Uteuzi wa Yawar kutamaliza mzozo wa kisiasa katika baraza la rais ambapo wadhifa wa rais umechukuliwa na kiongozi wa waasi wakikurdi Jalal Talabani na wadhifa wa makamu wa pili wa rais ukipewa mshia Adel Abdel Mahdi.
Wakati huo huo waziri wa kutetea haki za binadamu nchini humo amesema rais wa zamani wa nchi hiyo Saddam Hussein pamoja na waliokuwa wasaidizi wake wanatazama kikao hicho kupitia runinga.
Hatua hiyo inalenga kutoa ujumbe kwa rais huyo kwamba utawala wake umekwisha na kwamba Iraq iliyoko hivi sasa iko chini ya utawala mpya.