BAGHDAD. hali ya Iraq bado haijabadilika.
3 Mei 2005Wanajeshi wa Marekani nchini Iraq wamewauwa watu 12 na kuwajeruhi wengine wawili akiwemo mtoto wa miaka sita kufuatia mapigano makali katika mji wa Qaim karibu na mpaka Syria.
Habari azaidi zinasema kuwa wanajeshi sita wakiongozwa na wanajeshi wa Marekani wamejeruhiwa katika pambano hilo.
Miongoni mwa vitu vilivyokamatwa na ambavyo vinashukiwa kuhusika na wafuasi wa kundi la kigaidi La Al Qaeda nchini Iraq linaongozwa na Abu Musab al – Zarqawi ni vitambulisho vya bandia na pesa za kigeni.
Kwingineko msako wa kuwatafuta marubani wawili wa ndege za kivita za Marekani bado unaendelea.
Ndege hizo ambazo zilikuwa mazoezini yahofiwa ziligongana kutokana na hali mbaya ya hewa.
Wataalamu wameripoti kuwa hakuna dalili ya moto mkubwa uliozuka baada ya ajali hiyo.
Wakati huo huo Lyndie England mwanajeshi wa Marekani aliegonga vyombo vya habari tangu mwaka jana katika kesi ya unyanyasaji wa wafungwa katika jela ya Abu Ghraib nchini Iraq amekiri makosa saba kati ya tisa aliyoshtakiwa katika mahakama moja mjini Texas Marekani.
England anatarajiwa kupokea kifungo cha hadi miaka 11 iwapo atapatikana na hatia.