Baghdad. Hali ya hatari yarefushwa nchini Iraq kupambana na wimbi la mashambulizi.
14 Mei 2005Matangazo
Waziri mkuu wa Iraq Ibrahim al Jaafari amerefusha kipindi cha hali ya hatari ambayo iliwekwa nchini humo mwaka uliopita. Tangazo hilo linakuja wakati kuna wimbi jipya la mashambulizi wiki hii ambalo limesababisha vifo vya zaidi ya watu 100.
Sheria zinazoweza kutumika kwa dharura, zinaruhusu serikali kuchukua hatua za kuwazuwia wananchi kutembea usiku, kufunga mipaka na viwanja vya ndege , na kuwaweka kizuizini watuhumiwa bila ya kufuata hatua za kawaida za kisheria.
Wapiganaji wa chini kwa chini wamezidisha kampeni yao ya kulipua mabomu ya kijitoa mhanga pamoja na mashambulio mengine katika juhudi za kuidhoofisha Iraq.