Baghdad. Bunge la Iraq lapewa muda zaidi kukamilisha katiba.
26 Agosti 2005Matangazo
Spika wa bunge la Iraq amesema kuwa muda wa mwisho uliopangwa kukamilisha majadiliano juu ya namna ya kuandika muswada wa katiba ya nchi hiyo umeongezwa kwa muda wa saa 24.
Hajim al-Hassan ametoa tamko hilo muda mfupi tu baada ya muda wa kwanza kumalizika.
Muswada huo umewasilishwa katika bunge siku ya Jumatatu, wiki moja baada ya muda uliopangwa hapo kabla kupita.
Wabunge kutoka makundi ya Washia na Wakurdi walikubaliana juu ya vipi katiba hiyo iandikwe lakini wale wanaotoka katika kundi la Wasunni hawakukubali.
Al Hassan baadaye aliwapa siku tatu zaidi ili kuweza kumaliza tofauti zao , lakini hadi sasa hawajaweza kufanya hivyo.