BAGHDAD : Bunge la Iraq kukutana Jumamosi
22 Machi 2005Matangazo
Bunge la Iraq litakutana Jumamosi kumchaguwa Spika na kujaribu kufikia makubaliano juu ya serikali ili kumaliza mzozo wa kisiasa nchini humo.
Kikao cha kwanza cha kazi cha bunge hilo kitafanyika mwishoni mwa mwa juma baada ya vyama vya makundi ya Washia na Wakurdi ambao baina yao wana wingi wa theluthi mbili ya viti bungeni unaohitajika kuunda serikali kusaini azmio juu ya hatima ya mji unaozalisha mafuta wa Kirkuk na dhima ya Uislamu.
Mjumbe wa kundi la Mashia la United Iraq Alliance amesema watayakinisha haja ya kutatuwa mizozo ya maeneo kwa mujibu wa katiba ya mpito ambayo pia inasema Uislamu ni chanzo kikuu cha utungaji wa sheria na kuondosha hofu kwamba Iraq itatawaliwa na masheikh.