BAGHDAD: Bomu la gari limewaua polisi na raia
2 Aprili 2005Matangazo
Askari polisi 4 na raia mmoja wameuawa nchini Iraq katika shambulio la bomu la gari lililofanywa na mtu aliejitolea kufa.Shambulio hilo limetokea mjini Khan Bani Saad kaskazini mwa mji mkuu Baghdad.Bomu hilo lilifichwa katika gari na kuripuliwa,polisi walipokwenda kuikagua gari waliyoiona kuwa ni tupu.Polisi wote 4 na raia aliekuwa akipita na gari waliuawa.Watu wengine 2 pia yasemekana kuwa walijeruhiwa katika shambulio hilo.