BAGHDAD: Balozi mdogo wa Pakistan atoweka Iraq
10 Aprili 2005Matangazo
Mwanadiplomasia wa Pakistan ametoweka katika mji mkuu wa Iraq,Baghdad.Msemaji wa polisi nchini humo amesema familia yake ilripoti kwa polisi baada ya mwanadiplomasia huyo kutorejea nyumbani kutoka sala za jioni siku ya jumamosi.Ubalozi wa Pakistan umesema haujuwi kile kilichomfika balozi mdogo Malik Mohamed Javed.