Baghdad: Baada ya ziara ya ghafla ya Rais George Bush wa Marekani nchini Iraq hapo jana, ...
29 Novemba 2003Matangazo
seneta wa mkoa wa New York, Bibi Hilary Clinton, amemaliza kuyatembelea majeshi ya nchi yake yalioko katika mji mkuu wa Iraq. Mke huyo wa rais wa zamani alitaka kufikiriwe upya juu ya siasa ya kigeni ya Marekani. Alisema kutokana na hali ya usalama ilio ya hatari na matatizo ya kuandaa kukabidhi madaraka kwa viongozi wa Iraq, mzozo wa Iraq lazima ushughulikiwe kimataifa. Kwa sasa Marekani inahitaji sana msaada kutoka jamii ya kimataifa.
<br><br>
Kwa upande mwengine, mshauri wa masuala ya usalama wa taifa huko Marekani, Bibi Condeleeza Rice, aliarifu kwamba Marekani haikatai tena juu ya kufanyika uchaguzi wa moja kwa moja kuichaguwa serekali ijayo ya mpito ya Iraq. Mtawala wa kiraia wa Marekani katika Iraq, Paul Bremer, anafanya mazungumzo na Washia wa Iraq juu ya suala hilo. Jana katika hujuma iliofanywa katika kambi ya kijeshi mjini Mossul, kaskazini ya Iraq, mwanajeshi wa Kimarekani aliuliwa.