BAGHDAD: Askari wa Japani kuwasili Iraq
20 Januari 2004Matangazo
Kundi la kwanza la askari wa Japani limewasili kusini mwa Iraq kwa maandalizi ya mapokezi ya wanajeshi wake 600 wanaoletwa kusaidia harakati za ujenzi mpya wa nchi hiyo. Hii imekuwa mara ya kwanza tangu kumalizika vita vya pili vya dunia kwa Japani kutuma askari wake katika nchi ambayo mapigano bado yanaendelea. Askari hao watahusika na kazi zisizokuwa za kijeshi kama huduma za afya na mambo mengine kama usambazaji wa maji safi ya kunywa, ukabarati wa majengo yalioharibiwa na vita au usafirishaji wa vifaa.