Baghdad. Afisa wa ubalozi wa Misr nchini Iraq atekwa nyara.
4 Julai 2005Afisa wa ngazi ya juu wa ubalozi wa Misr nchini Iraq ametekwa nyara mjini Baghdad. Wanadiplomasia wa Misr wamesema kuwa Ihab el Sherif, ambaye ni kiongozi ubalozi wa Misr nchini Iraq , alikamatwa na watu wenye silaha waliokuwa katika magari mawili wakati akinunua gazeti karibu na nyumbani kwake siku ya Jumamosi jioni.
Hakuna taarifa zozote kuhusu wapi aliko hadi sasa.
Duru za kidiplomasia na polisi zinasema kuwa utekaji nyara huo unaweza kuwa ni kutokana na taarifa ambazo hazijathibitishwa katika muda wa wiki iliyopita kuwa al Sherif atakuwa balozi wa kwanza kutoka taifa la Kiarabu katika nchi hiyo inayoongozwa na serikali inayoungwa mkono na Marekani.