BAGDAD: Watu 30 wakutwa wamekufa Iraq/Syria
9 Machi 2005Matangazo
Kiasi cha miili 30 ya watu imepatikana katika mpaka kati ya Iraq na Syria. Maafisa wa hospitali wamesema kuwa wahanga wamekuwa na majeraha ya risasi kichwani ama kifuani. Walikuwa na nguo za kiraia na wanafikiriwa kuwa wameuwawa katika muda wa siku kadha.
Mjini Bagdad, wakati huo huo, waasi wamefanya shambulio lingine karibu na hoteli moja ambayo inakaliwa na polisi na makandarasi kutoka nje ya nchi hiyo.
Watu wenye silaha baadhi wakiwa katika sare za polisi, wamewauwa walinzi wawili kabla ya gari moja la taka lililojazwa milipuko kugongwa katika eneo la kuegeshea magari. Kiasi cha watu wawili wameuwawa katika mlipuko huo na wengine 30 wamejeruhiwa.