Bagdad. Jenerali wa jeshi nchini Iraq auwawa kwa kupigwa risasi.
28 Machi 2005Matangazo
Nchini Iraq, kiasi cha watu 16 wameuwawa na wengine wengi wamejeruhiwa katika mashambulio mbali mbali tofauti. Generali wa jeshi la Iraq ameuwawa , na watoto wake wawili wamejeruhiwa katika shambulio la risasi katika eneo la kusini mashariki la mji mkuu Bagdad. Hapo mapema mtu mmoja amejilipua na kuwauwa makomandoo 11 maalum wa jeshi la Iraq na kuwajeruhi wengine wengi.
Wakati huo huo mwanasiasa wa ngazi ya juu wa madhehebu ya Shia amesema kuwa bunge la Iraq linapanga kukutana kesho kupiga kura kumchagua spika na wasaidizi wake wawili wakati majadiliano yanaendelea katika uundwaji wa serikali mpya.