Baerbock asema lengo la Putin ni kuiangamiza Ukraine
1 Aprili 2025Matangazo
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock amefanya ziara katika mji mkuu wa Ukraine, Kiev. Baerbock amesema lengo la rais wa Urusi Vladimir Putin linabaki kuwa ni kuiharibu na kuiangamiza Ukraine.
Baerbock ameyasema hayo akiwa katika ziara ya kuaga mjini Kiev ambako amesema mikataba yoyote ya madini adimu na Ukraine yanatakiwa yaendane na sheria ya Ulaya.
Alipoulizwa kuhusu uwezekano wa makubaliano kati ya Ukraine na Marekani kuhusu madini hayo, Baerbock amesema Ulaya ilikuwa tayari imeafikia mkataba na Ukraine na kwamba mkataba wowote mpya sharti uzingatie sheria ya Umoja wa Ulaya.
Baerbock amesema wanazungumza na wadau wote ipasavyo.