Baerbock aapa kuwa mpatanishi kuliongoza Baraza Kuu la UN
16 Mei 2025Baerbock mwenye umri wa miaka 44 ameyasema haya alipokuwa analihutubia baraza hilo huko New York jana.
Waziri huyo wa zamani aliyehudumu hadi wiki iliyopita serikali mpya ilipopatikana Ujerumani, ndiye mgombea wa pekee wa wadhfa huo mkuu.
Amesema pia kwamba kuna haja ya kufanyika mabadiliko katika Umoja wa Mataifa kutokana na machafuko mengi yanayoendelea katika sehemu tofauti kote duniani na shinikizo la kifedha linaloshuhudiwa.
Urusi imeonyesha pingamizi kwa baerbock kuchaguliwa katika nafasi hiyo.
Huku ikiwa wadhfa huo wa mwaka mmoja kama rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ukichukuliwa kutokuwa na umuhimu mkubwa, Baerbock huenda akashawishi michakato ya kufanya maamuzi.
Kura rasmi ya nafasi hiyo itakuwa Juni 2 na Baerbock atazinduliwa rasmi Septemba 9, muda mfupi kabla viongozi wa dunia kukusanyika huko New York.