Baba Mtakatifu ziarani Ujerumani na Abdu Mtullya
12 Septemba 2006Matangazo
Baba Mtakatifu Benedikt wa 16 amesema kumtukuza Mungu maana yake ni kumpa nafasi katika dunia na matendo yetu .Amesema tunapaswa kutumia muda zaidi kwa ajili ya Mungu na huo ndio msingi wa imani sahihi.
Baba Mtakatifu amesema hayo katika sala aliongoza mbele ya waumini alfu 60 katika mji wa Alötting katika jimbo la Bavaria.Ameeleza kuwa pale ambapo Mungu ni mkubwa, binadamu hatakuwa mdogo na dunia itang’ara.
Kiongozi huyo wa wakatoliki leo pia anatarajiwa kuongoza sala mbele ya waumini wapatao laki tatu katika mji wa Ragensburg.