Aznar azuru wanajeshi wa Kispania Iraq:
21 Desemba 2003Matangazo
BAGHDAD: Waziri Mkuu wa Uspania José Maria Aznar amevitembelea vikosi vya nchi yake nchini Iraq. Ni ziara ya kwanza kufanywa baada ya vita vya Iraq na Waziri Mkuu wa Uspania ambaye pamoja na Waziri Mkuu wa Uingereza Tony Blair wanaunga mkono bila ya masharti vita vya Iraq vinavyoongozwa na Marekani. Bwana Aznar alikutana na wanajeshi hao wa Kispania waliowekwa kama sehemu ya wanajeshi wa Kimataifa waliokabidhiwa majukumu ya hifadhi ya usalama katika maeneo ya Kusini wanakoishi zaidi Washiya wa Kiiraq. Uspania ina jumla ya wanajeshi 1300 nchini humo. Jumla ya Waspania kumi wamekwisha uawa Iraq katika mashambulio ya kigaidi. Hapo mwezi uliopita wa Novemba watumishi saba wa Shirika la Upelelezi la Uspania waliuawa Iraq.