Australia yapongeza mipango ya Ujerumani ya waomba hifadhi
10 Aprili 2025
Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Austria, amesema mapambano dhidi ya ulanguzi wa binadamu na matumizi mabaya ya mifumo ya kuomba hifadhi, yanaweza kupata ufanisi kupitia juhudi za pamoja.
Umoja wa Ulaya wapendekeza sheria ya kuharakisha kuwaondoa wahamiaji Ulaya
Siku ya Jumatano, muungano wa vyama ndugu vya kihafidhina wa Christian Democratic Union (CDU) na Christian Social Union (CSU), ulifikia makubaliano na chama cha siasa za wastani za mrengo wa kushoto Social Democratic (SPD), yanayojumuisha kifungu tata kinachoruhusu kukataliwa kwa waomba hifadhi kwenye mipaka na katika maombi ya hifadhi kwa ushirikiano na mataifa jirani ya Ulaya.
Ulaya yashutumiwa kuendesha vitendo vya unyanyasaji kwa wahamiaji wa Afrika
Akizungumzia kifungu hicho, msemaji huyo wa wizara ya mambo ya ndani ya Austria, amesema wana imani kwamba Ujerumani itatekeleza hatua hiyo katika mipaka ya ndani ya Umoja wa Ulaya kwa mujibu wa sheria.