Australia kuongeza msaada Gaza baada ya maandamano Sydney
4 Agosti 2025Matangazo
Waandaaji wa maandamano hayo ya Jumapili (Agosti 3) walikisia watu baina ya 200,000 na 300,000 walihudhuria, huku polisi ikiishusha idadi hiyo hadi 90,000.
Siku ya Jumatatu (Agosti 4), Waziri wa Mambo ya Kigeni, Penny Wong, alitangaza nyongeza ya dola milioni 13 na kuifanya nchi hiyo sasa kuwa imetowa jumla ya dola milioni 130 kwa Gaza na Lebanon, tanguvita vya Gaza vianze kufuatia uvamizi wa Hamas dhidi ya Israel mnamo Oktoba 7, 2023.
Wong alisema uamuzi huo unafuatia kufunguliwa kwa njia mpya za kufikishia misaada ya kiutu na Israel, wakati huu Umoja wa Mataifa ukisema Gaza inakaribia kutumbukia kwenye janga la njaa.
Zaidi ya Wapalestina 60,000 wameshauawa tangu Israel ianze mashambulizi yake kwenye Ukanda huo.