Miaka 80 iliyopita, tarehe 27 Januari 1945, wanajeshi wa Jeshi la Kisovieti walifika katika kambi ya mateso na maangamizi ya Auschwitz. Jinsi Auschwitz ilivyogeuka alama ya mauaji ya Wayahudi (Holocaust), mauaji ya kimbari, na ugaidi - na kuwa kituo kikubwa zaidi cha kambi kilichojengwa na Ujerumani ya Kinazi.