AU: Mkataba wa amani kati ya DRC na M23 ni "hatua muhimu"
19 Julai 2025Matangazo
Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Afrika Mahmoud Ali Youssouf ameongeza kuwa hatua hiyo inaashiria ufanisi wa juhudi zinazoendelea za kufikia amani ya kudumu, usalama, na utulivu mashariki mwa Kongo na katika eneo zima la Maziwa Makuu.
Mpango huo umesainiwa Jumamosi mjini Doha kati ya wajumbe wa serikali ya Kongo na wale wa kundi la waasi la M23 baada ya miezi kadhaa ya mazungumzo yaliyosimamiwa na Qatar huku Marekani ikizidisha pia shinikizo.
Kwa zaidi ya miongo mitatu, eneo la Mashariki mwa Kongo limekumbwa na vita ambavyo vimeongezeka katika miaka ya hivi karibuni kufuatia kusonga mbele kwa waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda.