Atiwa nguvuni Ujerumani
20 Agosti 2006Matangazo
BERLIN:
Polisi wa ujerumani wamemtia nguvuni mtu anaetiliwa shaka kuhusika na jaribio la mwezi uliopita la kuripua mambomu katika magari 2 ya m oshi ya abiria.
Mlebanon huyo mwenye umri wa miaka 21 alitiwa nguvuni katika kituo kikuu cha gari-moshi mjini Kiel,kaskazini mwa Ujerumani.
Wakuu wa usalama wanasema, wanaamini yamkini akawa ni mmoja kati ya watu 2 walioonekana katika kamera katika stesheni kuu ya reli ya mjini Cologne,Julai 31.Hiyo ni siku ambayo mabomu hayo yalioshindwa kuripuka yalipogunduliwa ndani ya treni za abiria mjini Dortmund na Koblenz pamoja na taarifa zilizoandikwa kwa luigha ya kiarabu.
Mtuhumiwa huyo anafikishwa leo mahkamani.Polisi ingali inamsaka mwengine.