Ujerumani imetangaza kusitisha kuiuzia silaha Israel ambazo huenda zikatumika katika Ukanda wa Gaza, kufuatia uamuzi wa Israel kutanua operesheni zake katika ukanda huo. Tangazo hilo limetolewa Ijumaa mjini Berlin na Kansela Friedrich Merz. Ili kufahamu ukubwa wa tangazo hili, Jacob Safari amezungumza na mchambuzi na mtaalam wa siasa za Ujerumani Abdu Mtullya na kwanza alikuwa na haya ya kusema.