Madawa ya kuua wadudu hasa yale yanayotumika kwenye kilimo yanaendelea kuwa tishio kubwa kwa uzalishaji wa asali nchini Rwanda. Ingawa lengo la madawa hayo ni kulinda mazao dhidi ya wadudu waharibifu, athari zake kwa nyuki ni hasi na zinaweza kudhoofisha sekta nzima ya ufugaji wa nyuki. Sylivanus Karemera anasimulia katika Makala ya Mtu na Mazingira.