Aston Villa ina matarajio makubwa dhidi ya PSG
9 Aprili 2025Matangazo
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Paris kabla ya mechi hiyo Emery amesema Aston Villa ni klabu ya kihistoria iliyoshinda Kombe la Ulaya mwaka 1982 na bila shaka ni ya kipekee.
Soma pia: Bayern waangukia pua, Arsenal waishangaza Madrid
Villa iliishinda Club Brugge na kufika hatua ya nane bora, baada ya kumaliza katika nafasi ya nane bora na kukabiliana na PSG ambao waliwaondoa Liverpool kwa mikwaju ya penalti katika raundi ya mwisho kunaahidi kuwa mtihani mgumu zaidi kwa Villa.
Soma: Arsenal yatoa fursa kwa timu tano za England
Katikan mechi nyengine wawakilishi wengine wa Ujerumani Borussia Dortmund watakuwa ugenini kukipiga na Barcelona.