Nchini Tanzania viongozi wa kidini walitumia ibada za sikukuu ya Pasaka kutoa wito wa kufanyika uchaguzi huru, wa haki, na wenye kuheshimika wakikemea kile walichosema ni viashiria vya wazi vya uchaguzi huo nao kuharibiwa. Mohammed Khelef amezungumza na Askofu Benson Bagonza, wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, KKKT, Dayosisi ya Karagwe, na anaeleza sababu ya yeye kutoa msimamo huo.