MigogoroAfrika
Shambulizi la wanamgambo lauwa askari sita Benin
17 Februari 2025Matangazo
Taarifa hizo zimetolewa na msemaji wa jehsi la Benin Ebenezer Honfoga alipozungumza na shirika la habari la Reuters. Amesema mkasa huo uliotokea siku ya Jumamosi ulishuhudia pia wanamgambo 17 wakiuawa.
Unafuatia mauaji ya wanajeshi kadhaa yaliyotokea mwezi Januari katika wilaya ya kaskazini ya Alibori inayopakana na mataifa mawili yanayohangaishwa na makundi ya itikadi kali ya Niger na Burkina Faso.
Soma pia:Kundi la kigaidi JNIM ladai kuhusika na shambulio la Benin
Benin na taifa jirani la mwambao wa bahari ya Atlantiki la Togo yameshuhudia mashambulizi kadhaa miaka ya hivi karibuni kufuatia kujitanua kwa wanamgambo wenye mafungamano na makundi ya itikadi kali ya Al-Qaeda na lile linalojiita Dola la Kiislamu.