Askari 7 wa Israel wajeruhiwa kufuatia mashambulizi ya Iran
14 Juni 2025Mzozo huo umeleta taharuki huku Israel ikionya kuwa mji mkuu wa Tehran "utawaka moto" endapo Iran itaendelea kuvurumusha makombora ya masafa kuelekea Israel.
Katika hatua nyingine, shirika la habari la Tasnim na televisheni ya taifa ya Iran, vimeripoti kwamba wanasayansi wengine watatu wa nyuklia wa Iran wameuawa kwenye mashambulizi ya Israel.
Wanasayansi wengine sita wa nyuklia waliripotiwa kuuawa katika mashambulizi ya Israel mapema siku ya Ijumaa.
Vyombo vya habari vya Iran, pia vimeripoti kwamba Tehran imeziarifu Ufaransa, Uingereza na Marekani juu ya uwezekano wa mashambulizi katika siku zijazo endapo zitaendelea kuunga mkono juhudi za ulinzi za Israel.
Vituo vya kijeshi vya kikanda vya nchi washirika na meli katika Ghuba ya Uajemi na Bahari ya Shamu, vimetajwa kama shabaha ya mashambulizi hayo.Iran na Israel zaendelea kushambuliana kwa makombora
Wakati huo huo afisa mmoja wa Iran amesema nchi hiyo ilihamisha vifaa vyake muhimu na vya kimkakati kutoka kwenye kituo chake cha nyuklia cha Fordo kabla ya Israel kukishambulia.